DW yazindua makala mpya za "Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani"

Mfululizo wa Makala Mpya za “Kivuli cha Ukoloni wa Ujerumani” unamulika jukumu la Ujerumani katika historia ya Afrika. Vipindi kumi vinaelezea namna Ujerumani ilivyojiunga na kinyang'anyiro cha kuigawanya Afrika.

DW imezindua mradi wake mpya wa mfululizo wa makala kuhusu historia ya Ujerumani ambazo zinaangazia sifa ya ukoloni wa Ujerumani barani Afrika. Kupitia mtazamo wa Kiafrika, vipindi kumi vinaelezea jinsi Ujerumani ilivyokuja kujiunga baadaye katika kinyang'anyiro hicho, ilivyokumbana na upinzani mkali, na ilivyojihusisha na unyanyasaji na ukatili. Vidio na vipindi hivi vya redio pia vinaangalia jinsi ukoloni wa Ujerumani unavyoendelea kuwepo katika maisha ya sasa.

Hafla ya kufana ya uzinduzi wa mradi huu mpya ilifanyika jijini Dar es Salaam Desemba 14, 2023 na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu na watalaamu wa historia.

image