Marekani yatangaza mpango wa ulinzi katika bahari ya Shamu

Marekani na mataifa mengine kadhaa yanaunda jeshi ili kuzilinda meli zinazopita kwenye bahari ya Shamu ambako zimekuwa zinashambuliwa kwa droni na makombora kutokea maeneo ya nchini Yemen yanayodhibitiwa na Wahouthi.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, amesema hayo nchini Bahrain.

Ukubwa wa mashambulio hayo ambayo baadhi yameharibu vyombo vya baharini, yamesababisha kampuni kadhaa za usafirishaji kuchukua hatua za kuepusha meli zao kupitia kwenye mlango wa bahari wa Bab el-Mandeb hadi hali ya usalama itakaposhughulikiwa.

Chini ya mkakati huo mpya meli za kijeshi zitaongeza uwepo wake kwenye eneo la bahari hiyo ya Shamu na kujiweka katika namna ya kuweza kuzilinda meli za biashara.

image