Baraza la Usalama la UN kupiga kura kuhusu Gaza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa bado linatatizika kupata kauli moja kabla ya kura inayotarajiwa hii leo Jumanne (19.12.2023) kuhusu azimio jipya la kutaka kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza
Azimio hilo pia ni la kuitaka Israel na Hamas kuruhusu kuingia misaada katika Ukanda huo kupitia nchi kavu, baharini na angani.

Azimio hilo linataka pia kuanzishwa kitengo cha Umoja wa Mataifa kitakachosimamia na kufuatilia misaada hiyo ya kibinadamu itakayotolewa.

Kura ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kusitisha mapigano Gaza yaahirishwa

Kura hiyo iliyokuwa ifanyike hapo jana Jumatatu iliahirishwa kutokana na mazungumzo yanayoendelea juu ya maneno sahihi yanayofaa kutumika kwenye rasimu ya azimio hilo.

image