Watu 118 wafa kutokana na tetemeko China

Watu wapatao 118 wamekufa kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea usiku wa kuamkia leo (19.12.2023) kwenye maeneo ya milima ya kaskazini magharibi mwa China.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, maafa hayo ni makubwa kabisa kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 10 nchini humo. Mamlaka za dharura katika jimbo la Gansu, zimetoa wito juu ya kupatikana wafanyakazi 300 wa ziada ili kukabiliana na maafa hayo.

Taarifa zinasema watu zaidi ya 500 wamejeruhiwa katika tetemeko hilo lililofikia nguvu ya 6.2.

Zaidi ya watu 100 wamepoteza maisha baada ya tetemeko la ardhi kupiga eneo la kaskazini magharibi mwa China

Nyumba na barabara zimeharibiwa. Pia nishati ya umeme pamoja na mawasiliano yamekatika. Wazima moto, wanajeshi na polisi 4,000 wamepelekwa kwenye sehemu ya maafa kufanya shughuli za uokozi.

image