Chadema Tanzania
Chadema Tanzania

Chadema Tanzania

@chadematanzania

Kenya: Wabunge kujadili mapendekezo ya utafutaji haki dhidi ya wanajeshi wa Uingereza nchini humo
Wabunge wa Kenya wanatazamiwa kujadili ripoti inayopendekeza mashtaka ya mauaji dhidi ya wanajeshi waliozuru Kenya yafunguliwe katika mahakama za nchini humo.

Pendekezo hilo litakalojadiliwa siku ya Jumanne, limo katika ripoti ya timu ya bunge inayopitia mkataba wa ushirikiano wa ulinzi kati ya Kenya na Uingereza.

Inafuatia ghadhabu ya umma baada ya madai kwamba wanajeshi wa Uingereza huenda walihusika katika mauaji ya Agnes Wanjiru - mwanamke Mkenya aliyepatikana amekufa mwaka wa 2012 baada ya kutumia tafrija ya jioni na wanajeshi.

Inafuatia ghadhabu ya umma baada ya madai kwamba wanajeshi wa Uingereza huenda walihusika katika mauaji ya Agnes Wanjiru - mwanamke Mkenya aliyepatikana amekufa mwaka wa 2012 baada ya kuwa katika tafrija ya jioni na wanajeshi.

Jeshi la Uingereza lilishutumiwa kwa kuficha ukweli, kwa mujibu wa ripoti ya Sunday Times, lakini Wizara ya Ulinzi ya Uingereza baadaye ilisema inashirikiana na uchunguzi wa Kenya kuhusu kifo hicho.

Wabunge nchini Kenya walio katika kamati ya ulinzi pia wanapendekeza kwamba wanajeshi wanaozuru walazimike kuhudumia jamii kupitia uwajibikaji wa kijamii wa shirika.

Walikutana na maafisa wa ubalozi wa Uingereza, maafisa kutoka wizara ya ulinzi na mashauri ya kigeni ya Kenya, pamoja na wapelelezi wanaochunguza mauaji ya Bi Wanjiru kabla ya kuandika ripoti hiyo.

Jeshi la Uingereza lina kitengo cha kudumu cha kufaya mazoezi katika mji wa kati wa Nanyuki chini ya makubaliano na serikali ya Kenya.

Imepakiwa mnamo 17:1317:13
Polisi Tanzania: Thabo Bester na mpenzi wake kurejeshwa Afrika Kusini
w
GALLO imagesCopyright: GALLO images
Mhalifu maarufu wa Afrika kusini Thabo Bester na mpenzi wake Dr Nandipha Magudumana hawataendelea na kesi yoyote katika mahakama ya Tanzania, watashtakiwa katika mahakama za Afrika Kusini.

Msemaji wa Polisi wa Tanzania, David Misime ameiambia BBC kuwa Bester na mpenzi wake huyo waliingia nchini kinyume cha sheria, lakini kwa mujibu wa sheria za kimataifa watafata utaratibu wa kuwarudisha Afrika kusini ili waendelee na mashtaka yao.

“Baada ya polisi wetu kupata taarifa zake na anayedaiwa kuwa mpenzi wake Dk Nandipha. Walikamatwa na bado wapo kizuizini. Tunakamilisha taratibu za kisheria kati ya nchi hizo mbili na tutamkabidhi kwa maafisa wa Afrika Kusini.

Siku ya Jumamosi Polisi walithibitisha kukamatwa kwa Thabo Bester, mpenzi wake Dk. Nandipha Magudumana, na Zakaria Alberto huko Arusha, Kaskazini mwa Tanzania.

Bester ambaye anajulikana kama "mbakaji wa Facebook" kwa kutumia mtandao wa kijamii kuwarubuni waathiriwa wake.

Alipatikana na hatia mwaka wa 2012 kwa kumbaka na kumuua mpenziwe mwanamitindo Nomfundo Tyhulu. Mwaka mmoja mapema, alipatikana na hatia ya kubaka na kuwaibia wanawake wengine wawili.

Alifanikiwa kutoroka gerezani na kuaminisha mamlaka za Afrika kusini kuwa alijiua kwa moto katika chumba chake cha gereza.

Wakati huo huo, Askari wa gereza aliyesimamishwa kazi na baba yake mpenzi wa Thabo Bester wanakabiliwa na msururu wa mashtaka yakiwemo mauaji, uchomaji moto na kusaidia kutoroka kwa Thabo Bester.

Kulingana na stakabadhi za mahakama, watu hao wawili wanadaiwa kumuua kimakusudi mtu asiyejulikana Machi mwaka jana.

Kesi yao imeahirishwa hadi Aprili 17 kwa uwezekano wa maombi ya dhamana, Wamewekwa rumande ya polisi.

Kampuni ya ulinzi inayomilikiwa na Uingereza ya G4s ilikuwa ikiendesha gereza alimofungiwa Bester. Tangu wakati huo imechukuliwa na maafisa wa magereza ya Afrika Kusini kufuatia kashfa yake ya kutoroka.

image

Lissu ataja mchawi wa ugumu wa maisha
Muktasari:
Makamu Wenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amesema ugumu wa maisha unaowakabili wananchi hivi sasa umesababishwa na Katiba iliyopo.

Dar es Salaam. Wakati malalamiko ya ugumu wa maisha yakiendelea kutamalaki nchini, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amesema kupanda kwa bei ya chakula na bidhaa mbalimbali kutakomeshwa kama Tanzania itapata Katiba mpya.
Lissu aliyerejea nchini leo, Januari 25, 2023 kutoka Ubelgiji alipokuwepo kwa miaka mitano, amesema licha ya kutokuwa na uwezo wa kushughulika upandaji wa gharama lakini hatakoma kulizungumzia.

Lissu ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Januari 25, 2023 jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Bulyaga uliopo Temeke wakati wa mkutano wa hadhara wa kumpokea baada ya kurejea nchini akitokea Ubelgiji alikokuwa akiishi tangu mwaka 2018.
"Nataka nijitetee kwamba mimi sina mamlaka kisheria ya kupunguza bei hiyo, sina. Isipokuwa kuyazungumza tu... Kuyazungumza tu, hiyo nitaifanya haihitaji niwe na kacheo fulani," amesema.

Amesema ugumu wa maisha ni tatizo la kimsingi la kisiasa, kwani Mungu hajaamuru yote yanayofanyika bali ni mambo ya kibinadamu na kisiasa.

"Kwa sababu ni mambo ya kisiasa tuna mamlaka ya kuyaondoa, kwa hiyo kama umechoka kushindwa kununua maharage, sembe au tozo, hili liko ndani ya uwezo wetu, halihitaji maombi wala kumtishwa Mungu mambo yaliyopo kwenye uwezo wetu," amesema.

Ametoa kile alichokiita dawa ya matatizo hayo, kwamba itafutwe suluhu ya kisiasa itakayotokana na Katiba Mpya.

"Kwa wale wenye Katiba kuna kamstari mahali kwenye Katiba, kanakoelezea kwanini bei ya maharage ni sawa na bei ya nyama, Katiba inampa mamlaka makubwa Rais wa kuamua watu watozwe nini na kwa wakati gani" amesema.

Katika mkutano huo Lissu amesema Watanzania wanapaswa kuungana ili kudai Katiba mpya ili kuondoa matatizo yaliyopo hivi sasa.

image

Rais Samia ateua Ma-DC wapya 37, apangua 48
Muktasari:
Rais Samia Suluhu Hassan amepangua ya wakuu wa wilaya ambapo jumla ya wakuu wa wilaya 47 kote nchini wamehamishwa vituo vyao vya kazi.
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya wapya 37 na kuwahamisha vituo vya kazi wakuu wa wilaya 48 huku 55 wakibaki kwenye nafasi zao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 25, 2023 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunus, Rais Samia amefanya mabadiliko hayo na kuwateua wakuu wa wilaya wapya 37 huku wengine 47 wakihamishwa vituo vya kazi.
Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vyao vya kazi ni Suleiman Mwenda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba sasa atakuwa mkuu wa wilaya ya Monduli, mwingine ni Edward Mpogolo aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Same sasa atakuwa Mkuu wa wilaya ya Ilala.

Naye Halima Bulembo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza sasa ataongoza Wilaya ya Kigamboni, Hashim Komba aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea sasa ataiongoza Wilaya ya Ubungo.

“Mwanahamisi Mukunda aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Bahi sasa ni Mkuu wa wilaya Temeke, Saadi Mtambule aliyekuwa Mkuu wa wilaya Mufindi amehamishiwa wilaya ya Kinondoni, naye Sophia Kizigo aliyekuwa Mkuu wa wilaya Mkalama amehamishiwa wilaya ya Mpwapwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Godwe atakuwa Mkuu wa wilaya ya Bahi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Misungwi Veronica Kessy atahudumu wilaya ya Iringa.
Kwa aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Nzega ACP Advera Bulimba ataongoza Wilaya ya Biharamulo huku Majid Mwanga aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kilosa ataiongoza wilaya Mlele.

“Mkuu wa wilaya ya Magu, Salum Kali naye amehamishiwa wilaya ya Kigoma, Kisare Makori aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Uyui atakukuwa Wilaya ya Moshi, Mohamed Moyo aliyekuwa Wilaya ya Iringa atakuwa Mkuu wa Wilaya Nachingwea,” ilielezwa kwenye taarifa hiyo.
Wengine ni Kherry James aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo sasa ataiongoza wilaya ya Mbulu, Dk Vicent Anney amehamishwa kwenda Wilaya ya Bunda akitokea Wilaya ya Rungwe na Kanali Denis Mwila amepelekwa kuwa Mkuu wa Wilaya Mbarali akitokea Wilaya ya Ukerewe.

Mabadiliko hayo pia yamemgusa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawaga Sebastian Waryuba ambaye sasa kituo chake cha kazi ni Wilaya ya Malinyi, Danstan Kyobya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara sasa atahudumu kwenye nafasi hiyo kama Mkuu wa wilaya ya Kilombero.

Pia Dk Julius Ningu amehamishiwa Wilaya ya Ulanga akitokea wilaya Namtumbo naye Judith Nguli amehamishiwa Wilaya ya Mvomero akitokea Wilaya ya Liwale, Hanafi Msabaha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara.

“Luter Kanoni atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Wanging’ombe, Matiko Chacha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kaliua atahudumu Wilaya Misungwi, Ng’wilabuzu Ludigija aliyekuwa Wilaya ya Ilala sasa atahudumu wilaya ya Kwimba, Claudia Kitta kutoka Wilaya ya Masasai sasa atakuwa wilaya ya Wanging’ombe akitokea wilaya ya Masasi,” mabadiliko hayo yanaonyesha.

Aliyeguswa mwingine, Fatma Nyangasa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni sasa ni ataiongoza Wilaya ya Kisarawe na Nick John aliyekuwa wilaya hiyo amehamishiwa Wilaya ya Kibaha na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Halima Okash ataiongoza wilaya ya Bagamoyo.

Vilevile Filberto Sanga aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Mlele atahudumu Wilaya ya Nyasa na Ngollo Malenya aliyekuwa wilaya Ulanga sasa atakuwa Namtumbo, Simon Simalenga aliyekuwa Wilaya ya Songwe atahudumu wilaya ya Bariadi.
“Johari Samizi aliyekuwa wilaya ya Kwimba atahudumu wilaya Sinyanga,Anna Gidarya atahudumu wilaya ya Busega akitokea wilaya Ileje,Mosses Machali aliyekuwa wilaya Bukoba atahudumu wilaya Mkalama na Thomas Apson amehamishiwa wilaya ya Ikungi akitokea Siha,” alifafanua taarifa hiyo.

Mkeka huo pia umemgusa Kemilembe Lwota aliyekuwa Wilaya ya Biharamulo na sasa atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Joshua Nassari aliyehudumu Wilaya ya Bunda sasa ataendelea kuhudumu kwenye nafasi hiyo wilayani Iramba na Esther Mahawe amehamishwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbozi akitokea wilaya ya Kigoma.

Pia Simmon Chacha aliyekuwa wilaya ya Sikonge sasa ataiongoza wilaya ya Sikonge, Said Mtanda aliyekuwa Wilaya ya Arusha sasa atahudumu Wilaya ya Urambo na Dk Mohamed Chua chua aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Mbeya atahudumu Wilaya ya Kaliua.

Louis Bura atahudumu wilaya ya Tabora akitokea wilaya ya Urambo na Jokate Mwegelo aliyekuwa Wilaya ya Temeke sasa atahudumu Wilaya ya Korogwe, naye Albert Msando aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Morogoro amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni,

Pia Juma Irando amehamishwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza akitokea Wilaya ya Hai na Zainab Issa aliyekuwa Bagamoto sasa atahudumu Wilaya ya Pangani.

Wanaoendelea kubaki kwenye nafasi hizo ni pamoja na mkuu wa wilaya ya Karatu Dadi Kolimba, Raymond Mangwala (Ngorongoro), Dk Khamis Mkanachi (Konda) na Remedeus Emmanuel (Kongwa).

Wengine ni Jabir Shekimweri (Dodoma), Gift Msuya (Chamwino), Said Nkumba (Bukombe), Peres Magiri (Kilolo), Kanali Wilson Sakullo (Misenyi), Kanali Mathias Kahabi (Ngara) na Jamila Kimaro (Mpanda).
Pia yupo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu, Kanali Michaeli Ngayalina (Buhigwe), Kamali Evance Mallasa (Kakonko), Kanali Aggrey Magwaza (Kibondo),Kanali IssackMwakisu (Kasulu), Kanali Hamis Maiga (Rombo), Abdallah Mwaipaya (Mwanga) na Shaibu Ndemanga (Lindi).

Kazi atakayoifanya Lissu hadharani
Muktasari:
Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amesema kazi kubwa atakayoifanya baada ya kurejea nchini akitokea Ubelgiji ni kutengeneza nguvu ya umma kwa ajili ya Taifa ili ipatikane Katiba mpya.Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amesema kazi kubwa atakayoifanya baada ya kurejea nchini akitokea Ubelgiji ni kutengeneza nguvu ya umma kwa ajili ya Taifa ili ipatikane Katiba mpya.
Lissu ametoa kauli hiyo leo Jumatano, Januari 25, 2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Bulyaga wilayani Temeke ambapo pia ulikuwa kwa ajili ya kumpokea.

"Mwenyekiti wetu na chama chetu tulipata nafasi ya kuzungumza na Rais Samia Suluhu Hassan na akakubali tuzungumzie mambo yetu na mustakbali wa Taifa letu, huko nyuma kwa hayati Magufuli ilishindikana” amesema.
Amesema wataendelea na mazungumzo hata yeye amechangia katika mazungumzo yaliyokuwa yanafanyika lakini kinachotakiwa ni kupatikana kwa Katiba mpya.

"Tukiamua tutapata Katiba mpya kabla ya mwaka 2025 na Tume hintapatikana kama Katiba mpya itapatikana,"

Amesema endapo watamsadia Mbowe katika kudai katiba inawezekana lakini kama Watanzania watalegalea haitawezekana.

"Tukijenga shinikizo lenye nguvu kweli tutapata Katiba mpya kabla ya mwaka 2025 na tukipata hiyo tutapata Tume huru ya Uchaguzi, tume haiundwi nje ya Katiba," amesema.

"Tutafute namna ya kuhakikisha wote wanaoumizwa na utaratibu huu, ili tumpe nguvu Mwenyekiti na timu yake ya kwenda kudai kwenye hayo mazungumzo," amesema.

image

Mbowe awatwisha zigo wakazi wa Dar

Muktasari:
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema miji mikubwa dunia ndiyo kitovu cha mageuzi yanayofanyika

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema mageuzi ya siasa za Tanzania yanapaswa kuanzia Dar es Salaam kwa kuwa ndilo jiji lenye idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mbowe ambaye ni aliwahi kuwa Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na mbunge wa Hai, amesema nchi zote zinazojitambua kidemokrasia, majiji ndiyo huongoza kwa mageuzi hivyo Dar es Salaam inapaswa kuwa kitovu cha mageuzi.

Kauli hiyo ameitoa leo Jumatano Januari 25, 2025 katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika viwanja vya Bulyaga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam ambapo pia ni wa kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu aliyekuwapo nchini Ubelgiji.
"Kutokana na idadi kubwa ya watu waliopo Dar es Salaam kama wakiamua kudai Katiba mpya kwa kushirikiana utafika wakati Katiba mpya itapatikana. Mwaka huu tumefungua mikutano, tumerejea leo Dar es Salaam kumpokea Makamu, tutapiga jaramba, huku tunazungumza na kuwaamsha wananchi,"

"Inashangaza kuona Tanzania inaongozwa na chama kimoja katika kipindi cha miaka 30 ya vyama vya siasa, leo Rais ameteua wakuu wa wilaya mnaambiwa leo huyu ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke hamumjui hajawahi kuomba kura," amesema.

Mbowe pia amesema kama Chadema ikipata fursa ya kuongoza Tanzania watahakikisha kiongozi yeyote wa kisiasa hatopewa wajibu kwa kuteuliwa bali atachaguliwa na wananchi.

image